Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba 22, 2017

MATIBABU YA UGONJWA WA KUZIBA SIKIO.[CERUMEN IMPACTION]

Picha
  katika hali ya kawaida sikio la binadamu hutengeneza utando unaovutika kama asali, utando huu huzuia uchafu kuingia ndani ya sikio, kulainisha sikio na kukamata wadudu wanaoingia ndani ya sikio..utando huu hutengenezwa kwa kiasi kidogo sana kwa siku ili kukizi mahitaji ya sikio kwa siku lakini katika hali isiyo ya kawaida utando huu unaweza kua mwingi sana na kuziba sikio na kumfanya mtu ashidwe kusikia vizuri. sio hivyo tu kuna sababu zingine mbalimbali ambazo zinaweza kuziba sikio la mtu na kulifanya lishindwe kusikia kama ifuatavyo.. matumizi ya vitu vya kuchokonoa sikio kama viberiti, kalama au pamba za masikioni. kuziba kwa nywele ambazo hupatikana ndani ya sikio. kuishi sehemu yenye vumbi sana matatizo ya mirija ya masikio kitaalamu kama auditory canal   dalili za kuziba kwa sikio maumivu makali sikioni kushindwa kusikia kuwashwa sikioni kusikia kama sauti za kengere sikioni. kizunguzungu   vipimo vipi hufanyika? kwa kifaa maalumu kwa jina la otoscope ...