DALILI ZA UGONJWA WA FIGO.
Kuharibika kwa chujio ama Glomerulonephritis ni aina ya ugonjwa wa figo unaoathiri sehemu maalum ya figo (chujio) inayohusika na uchujaji wa maji pamoja na uchafu kutoka katika damu. Sehemu hii huitwaglomelurus au chujio kama tutakavyokuwa tukitumia katika mada hii. Visababishi Mara nyingi chanzo halisi cha kuharibika kwa chujio za figo(glomerulonephritis) huwa hakijulikani. Hata hivyo wakati mwingine uharibifu huu unaweza kusababishwa na kushambuliwa na mfumo wa kinga ya mwili. Uharibifu katika chujio husababisha damu pamoja na protini kuingia katika mkojo. Tatizo hili hukua kwa haraka na figo linaweza kupoteza uwezo wake wa kuchuja maji na uchafu kwa kasi ndani ya muda mfupi wa kati wiki chache mpaka miezi kadhaa. Aina hii ya kuharibika kwa chujio za figo kwa haraka hujulikana kitalaamu kama rapidly progressive glomerulonephritis. Ukubwa wa tatizo na vihatarishi vyake Takribani robo ya watu wanaopatwa na tatizo sugu la glomerulonephritishuwa hawana historia ya kuwa...